sound on
Moza
Helen Paul
Sura 01
Sura 02
Sura 03
Sura 04
Sura 05
Sura 06
Sura 07
Sura 08
Sura 09
Tansania
Moza Helen

Nakala

Hi Nathalie. Habari yako? Mimi naitwa Moza Said Salim kutoka Pemba. Napenda kujibu masuali yako kwa lugha ya Kiswahili sasa.

Naomba unisikie. Suala la kwanza uliniuliza ni vipi nilijuana naye Helen Paul. Helen Paul nilianza kujua naye kuanzia 1992 wakati tulipokutana katika kufanya kazi kwenye mradi wa Kingereza unawaitwa ZELIP ambao ni Zanzibar Language Improvement Project. Mradi huu ulikuwa chini ya British Council. Sasa yeye alikuwa na VSO wakati huu na mimi nilikuwa mwalimu wa primary school. Nilichaguliwa na Wizara kufanya kazi naye. Kuwasaidia walimu wa Kiingereza kwenye kazi zao katika ufundishaje.

Suala la pili. What is your relationship with Helen? Nilikua mahusiano yetu yaliku wakati gani na yalikuwa ni mna gani? Mahusiano yetu na Helen yalikua ni katika mazingira ya kazi. Kwenye huu mradi wa Kiingereza. Yeye alikuwa ni mkufunzi wa walimu wa Kingereza, yaani teacher trainer ELT (English Language in-service teacher training) na mimi nilikuwa mwalimu ambaye namsaidia kufanya kazi naye. Wakati huo kama vile kuendesha seminars kwa kuendesha mobile library, kuanzisha mobile library katika sehemu za vijijini kwa sababu walimu waliokua walikaa mbali sana katika vijiji waliokua na shida kuja katika mjini kutumia library. Kwa hivyo tulifanya mobile library kwa kupitisha katika skuli za vijijini ili wanafunzi wapate kufaidika kwa wakati huo kusoma vitabu na kuimprove Kiingereza chao.

Pia tuliawapa mafunzo walimu na baadaye kuangalia darasani wanazo wanazitumia methods kwenye ufundishaji kwa baadaye kufanya evaluation trainings zetu.

Zaidi ya hapo ni kwamba mahusiano yetu hasa. Yalizidi kwa ajili yali ....... mahusiano ilikuwa kubwa tumezoeana kama yeye ni ndugu, rafiki, au ndugu na alikuwa katika jamaa zangu na watoto wangu alikuwa amelewa sana. Kwa hivyo muhusiano alikua nzuri hapo katika kazi na familia na relatives yangu.

Suala la tatu. Vipi ilianzishwa hii Sisi Pamoja huko Pemba. Mimi kwa ulewa wangu jumia hii ya Sisi Pamoja kutoka Ujerumani. Basi nilielewa pale ambapo nilianzisha skuli yangu binafsi katika kijiji nashoishi. Na hapo nilikuwa nakabiliana na changamoto nyingi katika kuanzisha hiyo skuli lakini kwa juhuri yangu kubwa na hamu kubwa kufanya kazi na pia kwa vile vile walikuwa wajamii wako tayari kujiunga na skuli yangu ili watoto wako wasome hapo; basi Helen aliona ananisaidia. Alikuwa alinisidia pesa kidogo ambazo zinaniwezesha tutumia kwa ajili ya kununua na kufanya vifaa vya kufundishia. Vile vile ilikuwa akanisaidia kununua vitu kama tenki za maji na mashine za kupandisha maji. Na vile vile ilikuwa alinisaidia kwa ajili ya kupata vifaa vidogo vidogo kutoka Ujerumani aliniletea ili niliwezesha kwa walimu wangu kutumia kwa ajili ya kufundishia. Kwa hivyo msaada huu unliniwezesha mimi kuifanya skuli yangu iwezi kuendelea. Na hakusita ya Mwaka moja alikuwa ananisaidia kila mara kwa sababu anona ile improvement ya ili skuli ipo. Tunaweza kufanya kazi vizuri na yeye ananipa msaada ili skuli inweze kudumu na kukabika kwa hivyo alinisaidia sana na mpaka sasa hivi skuli inasimama ni inakubalika Skuli ya Maandalizi ambayo inategemea tu, haini msingi wala hakuna skuli ya sekondari. Na huu nii Miaka wa kumi na moja.

Suala namba nne inasema hivi. Umepata maendeleo gani kutoka Sisi Pamoja baada ya kutoa mafunzo? Mimi kwa upande wangu na skuli yangu nimefaidika vizuri na mafunzo hayo pamoja na walimu wangu kwa ajili ya walimu wangu kubadilika katika ufundishaji kwa sababu wamepata mbinu bora na za kisasa ambazo zinawasaidia kuwa wao wanaweza kutumia ujuzi ule na kuwafundisha watoto ili kuweza kufahamu kinacho kimefundisha. Vile vile walimu walikuwa na situ sana kutumia Kiingereza yaani walikuwa hawezi kujua ni ipi lugha sahihi hasa.

Vile vile walijifunza kufanya vifaa vya kufundishia walifaidika kupata vifaa wenyewe vya kufundishia ambavo ni bure wanavipata wanvitumia. Tulikua tumepata machine ya lamination tulikuwa tunatumia sana na laminating pouches zile si rahisi kuharibika na kuchanika. Walimu walikuwa wanataka kila mwaka mafunzo yanaendele na tunaangalia mahitaji ya walimu hasa.

Nini tunahitaji ili kuwabadilisha ma kuwazidi kuboresha wanfunzi wa Pemba?

Mimi bado kitu nilichokiona ni kwamba hayo matumizi ya Kiingereza. Walimu wanahitaji wapati sana mafunzo ili wawezi kukabiliana na syllabus zao - ni muhtasari -na pia hawezi kukabiria reference, au text book wazisomi wazilewi ili wawezi kufundisha kwa sahihi.

Vili vile kitu kilichokuwa kinahitajika ni njia za fundishia ya kisasa inatakiwa programme kama zile za computer. Wanafunzi wengi hawajifunzi computer mpaka elimu ya sekondari; kwa hivyo hapa primary wanahitaji wanapata mafunzo ya computers ili wanawezi kusoma kwa njia ya kisisa. Technology bado ni ipo nyuma sana. Wanafunzi wafaidike kwa njia hiyo.

Sita. Kwa nini ikawa huu umoja wa Sisi Pamoja ni muhimu sana kwa skuli yangu ya Star na wanfunzi wangu?

Ndio umoja huu wa Sisi Pamoja ni muhimu kwa sababu napopata misaada kutoka Sisi Pamoja na kuwa nafaidika na kuweza kufanya mazingira ya skuli yangu na walimu wangu. Wawezi kufundisha na wanafunzi kujisikia

wapo kwenye mazingira nzuri ya kujifunza.

Vile vile walimu wanakuwa wanafaidika sana kwa sababu ikiwa yanatoka matatizo tunaweza kuwatua, tunapata funds, tunaweza kuondosha matatizo yetu ambaye ni muhimu sana. Zaidi ni kwamba wanafaidika wanafunzi na wanajamii ambao wanaishi katika mazingira magumu sana yaani wale wanafunzi wanonaishi katika broken homes. Hawa wanapata msaada watoto wao kusoma bure pale kwa kila mwaka. Kwa hivyo hii ni fursa kubwa sana kusoma bila ya kulipa kwa muda ya miaka miwili. Na wengi wao tunawafatilia wanafanya vizuri baada ya kumaliza miaka miwili.

Suala nane. Nini matumaini yangu juu ya huu umoja tunaye Sisi Pamoja mahitaji muda mna kuja mbele.

Kuna changamoto nyingi lakini nimeweka na tumaini yangu n'geweza kupata msaada ili niwezi kujenga skuli iliokuwa ni nzuri au kuextend building hii liniayo ili inaweza kuleta sura nzuri ya skuli.

Vile vile nilikua na matumaini kwamba nitaweza kufungua skuli ya msingi ili kuweza kuona maendeleo ya watoto wetu wanatoka Star wakingia primary na wakifanya mitihani yao na mna gani tuanweza kuona wanfaulu na Star imefanya kazi ya mna gani? Na sasa inabidi tunawafatilia katika skuli mbali mbali. Wanajamii wanapendelea sana keendeleza skuli yenyewe.

Pointi nyingine kubwa kwa muda si mbali sana ni usafiri uliokua salama kabisa itunahitaji sana kupata school bus ambaye italeta wanafunzi skuli yetu ambayo itapeleka wanafunzi skuli yetu. Ina watoto kutoka sehemu mbali mbali wanakuja hapa kusoma kutoka vitua wanapokaa

Hayo ni matumaini yangu ya baadaye mahusiamano mazuri ya Sisi Pamoja.

Ipi faida ya huu urafiki wa umoja wa Sisi Pamoja kwa skuli yangu na kwa kisiwa kizima kwa jumla. Kwa kisiwa kizima ni kwamba zili training zilitolewa zilisaidia sana na mpaka leo walimu wanauliza wenyewe. Hizo ni muhimu sana. Kwa sababu tunapotoa training, baadaye tunafanya follow-up na tunaangalia walimu waliokuwa wako weak na ndio kila mara tunazidi kuwachukua na wale waliokuwa wazuri tunawachukua tunafanya wao ni teacher trainers yaani kuwasaidia wenziwe wao. Mbali mimi na Bibi Helen na mwenzetu Bi Zainab sisi facilitators tunaofanya hiyo training ya trainers. Lakini tuliandaa chini kuwapata best teachers ambao wanatusaidia kufanya kazi districtwise au zonalwise, wanapita wanakwenda kwenye zone wanafanya discussion na walimu au wanafanya lesson observations, basi wale walimu wanakuwa pia wanafurahi ili kuweza kupata niongozo kutoka kwa wale trainers. Trainers wanawafatilia walimu katika maskuli lakini hapa inabidi tupate pesa za kuwapa hawa kwenda kufanya follow-up katika skuli. Na sisi wenyewe kuweza kwenda na kupata repoti ambao repoti hiyo tunaipeleka mpaka kwenye Wizara ya Elimu kuweza kujua hali halisi; kwa hiyvo tunaisaidia Wizara ya Elimu katika kufanya kazi zao na wao wanakubali kabisa na wanafurahi sana.

Nakala ya Helen Paul