Moza
Helen Paul
Sura 01
Sura 02
Sura 03
Sura 04
Tansania
Moza Helen

Nakala

Mimi ninaitwa Helen Paul na zamani sana nilizaliwa Uingereza. Sasa nimestaafu na kuishi Ujerumani.

Hapa Ujerumani tuna shirika ambalo linaitwa 'Sisi Pamoja - Gemeinsam mit Pemba Island e.V.'.

Pemba ni kisiwa kilichopo karibu na Tanzania Bara.

Nitaeleza historia ya shirika letu kwa ufupi.

Kama nilivyosema, mimi nilizaliwa Uingereza na huko nilifanya kazi kama mwalimu kwenye skuli ya msingi na zaidi ya hayo nilikuwa mwanasaikolojia wa elimu. Baadaye, mnamomwaka 1980, niliamua kusafiri duniani kwa muda mmoja mzima. Niliporudi nilifahamu kwamba nilitaka kukaa katika nchi ya kigeni kwa muda mrefu ili kuishi na kufanya kazi pamoja na watu wakule. Sikutaka tena kuendelea kuwa mtalii.

Kwa bahati nzuri nilipata kazi kwa njia ya VSO (Voluntary Service Overseas) kwenye Wizara ya Elimu, Zanzibar, Unguja. Nilisomesha saikologia ya elimu nan usomeshaji wa Kiingereza Taasisi ya Kiswahil na Lugha za Kigeni. (1984-1986). Wakati huo watalii hawakuwepo Unguja. Plastiki pia ilikuwa hamna. Nilipata kazi mara ya pili kupitia VSO Pemba (1990 -1992).

Niliwasaidia walimu wa Kiingereza ambao walisomeshema skuli za Msingi. Nilipofanya kazi Pemba nilifamiana na shoga yangu Moza Said Salum. Wakati huo Moza alikuwa akisomesha Kiingereza katika Skuli ya MsingiMadungu, Chake Chake. Sisi wawili pamoja tuliwasaidia walimu kuboresha usomeshaji wao na kuwapa moyo kutumia mbinu mpya zu kufundishia.

Niliporudi Ulaya nilitaka kuendelea kuwasaidia walimu huko Pemba. Marafiki zangu Ujerumani walinishauri kuanzisha shirika. Tulifanya hivyo mwaka 2010. Mwaka 2012 hadi 2014 nilikuwepo Pemba tena (tena VSO) nikiendelea na kazi yangu pa moja na Bi Moza. Katika shirika letu tulichagua miradi mbalimbali ya elimu kisiwani Pemba. Tulifadhili skuli ya chekechea ya Bi Moza, Star Nursery, Chake Chake. Hiyo ni skuli ya binafsi na wanafunzi mia moja wanafundishwa vizuri sana. Kweli ni skuli bora. Wanafunzi wote wanasoma hesabu, kusoma, Kiswahili, Kiarabu, Kiingereza na kadhalika.

Wanachama wengine wa shirika 'Sisi Pamoja' ni wafadhili ambao wanawalipia wanafunzi maskini au yatima ada zao za skuli kwa muda wa miaka miwili. Tunafadhili skuli mbili za pwani, Skuli ya Makoongwe na Skuli ya Shamiani Mwambe, kwa sababu hawapati msaada sana. Tukisafiri Pemba twakuja na pesa mfukoni na pesa hizo zinasaidia kuboresha elimu kwenye skuli za Pemba moja kwa moja; hakuna gharama za uendeshaji - Tukisafiri Pemba twalipa nauli wenyewe. Kwa sababu hii watu wengi wa Ujerumani hutusaidia.

Kuna miradi mingine muhimu. Kwa muda wa miaka kumi tunawashauri

walimu wa skuli za chekechea ambao wanasomesha Kiingereza. Bi Moza na Bi Zainab (mfanyakazi wa Idara ya Skuli za Maandalizi) hupanga mafunzo baada ya kuulizia matakwa ya walimu.

Tena tuna „trainers“ wenyeji kumi wa Kiingereza kwenye skuli za maandalizi kutoka sehemu zote za Pemba. Sisi hufundisha 'watrainers' kila mwaka na „watrainers“ vile vile huwafundisha na kuwasaidia wenzao. Tunafanya kazi tukishirikiana na Wizara ya Elimu na washauri wa Kiingereza na skuli wa maandalizi za Pemba. Walimu wengi wa skuli za chekechea hawajui Kiingereza vizuri na hawana mbinu nyingi za kufundishia. Kama vile hadithi, mazungumzo ya watu wawili au ya makundi, „roleplay“ na kadhalika. Kwa kujifunza mbinu mpya za kufundishia wanapata mawazo mapya kutayarisha vifaa vipya vya kufundishia. Ni muhimu watoto waanze mapema kusoma na kuzungumza lugha za kigeni.

Dini ya Wapemba ni Uislamu. Asilimia 99 ya Wapemba ni Waislamu. Na Wapemba hufuata dini sana. Zamani wanawake walikuwa wamevaa buibui. Leo wanawake huvaa hijabu, barakoa, glavu na soksi. Watu wa Pemba ni watu wema sana. Wanawasaidia wengine kwa furaha na wageni hukaribishwa kila wakati. Ninatamani kurudi Pemba tena. Watu wengi wa Pemba hawajui Kiingereza vizuri. Ukiisha na iki fanya kazi Pemba ni lazima uje naufahamu Kiswahili kuwasiliana vizuri na wenyeji. Ninakumbuka siku moja nilipomkuta mzee fulani sokoni. Alinisalima. Niliweza kumjibu nikiongeza, 'Habari zako? Watoto hawajambo? Habari za nyumbani? Vipi hali?'n.k. Yeye akasema, 'Yule bibi kweli anajua Kiswahili. Kiswahili na Kiingereza zinatofautiana kuhusu matumizi ya kauli.

Kwa mfano Kiswahili kinatumia kauli za kutendewa na kusabibisha zaidi kuliko Kiingereza.

Kuna tafauti kubwa zaidi ya matumazimi ya lugha bainan ya Kiswahili na Kingereza. Ujerumani watu hutoa maoni yao moja kwa moja. Pemba watu hutoa maneno mengi na kupendelea kutosema maneno moja kwa moja.

Lugha ndio kioo cha utamaduni na itikadi zake.

Nakala ya Helen Paul